WAFANYABIASHARA wa mbogamboga na matunda mkoani Morogoro wamekipingoza chama cha wazalishaji wa mbogamboga nchini (Tanzania Hortcultural Association) kwa jitihada za kuendesha semina kwa wazalishaji na wauzaji wa mbogamboga nchini kwa kulengo la kuwawezesha kuwa na ujuzi katika uzalishaji na masoko ya mazao ya mbogamboga.
Wakioongea na mbiu ya maendeleo mjini Morogoro, wazalishaji wa mbogamboga katika kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro wamesema kuwa , watashirikiana na TAHA ili kufikia malengo sanjari na kupata mbinu za kisasa za uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na kupata masoko ya uhakika .
Waemesema wnahitaji semina za mara kwa mara hasa katika uzalishaji wa mboga ambazo zinahimili ushindani wa soko katika ulimwengu wa soko huru.
Chama cha wazalishaji wa mbogamboga nchini TAHA kupitia kwa wataalamu wake wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA Bi Jacqueline Mkindi kinaendesha semina kwa wajasiliamali na Taasisi mbalimbali ikiwemo Jeshi la Kujenga Taifa ili kuwawezesha kuzalisha mazao ya mbogamboga yenye viwango na yatakayohimili ushindani wa soko.
No comments:
Post a Comment