WAKATI serikali kupitia wizara ya Utalii na Maliasili ikiweka mikakati ya kupambana na ujangili kwa kushirikisha wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi.Katika kipindi cha miezi miwili wilaya ya Manyoni, mkoa wa Singida zaidi ya tembo 35 wameuwawa na majangili.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida Bi Fatma Toufiq ameeeleza hayo leo katika kijiji cha Mitundo wilayani humo baada ya kukamata meno ya tembo yenye zaidi ya kilo 150 kufuatilia taarifa ya toka kwa raia wema.
Zoezi hilo la kuwakamata majangili hao lilifanikishwa na uongozi wa kijijii cha Mitundo likiongozwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho.
Mkuuu wa wilaya hiyo amesema ,hali ni mbaya kwani kama wilayani Manyoni pekee majangili ndani ya miezi miwili wameuwa tembo 35 je hali ikoje nchini?
Amefafanuakuwa, mapambano dhidi ya ujangili hayana budi kuwashirikisha wananchi waishio vijiji vinavyopakana na mbuga za wanyama na hifadhi za Taifa ili taarifa ziweze kuwafikia mamlaka husika.
Mapema jana msanii wa kizazi kipyamashairi Mrisho Mpoto alizindua wimbo wake unafahamika kwa jina la "niache niishi"ukiwa na lengo la kampeni ya kupambna na ujangili kwa njia ya sanaa ukiwataka majangili ukiacha tabia ya kuuwa tembo kwa lengo la kupata meno ili kujinufaisha kiuchumi.
No comments:
Post a Comment