Tuesday, April 1, 2014

ASILIMIA 59 ya kaya nchini zina uhakika wa kupata maji safi na salama nchini.

JITIHADA za serikali katika kufikia malengo ya milenia ya 2025  huenda yakafanikiwa baada ya asilimia 59  ya kaya nchini kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama, tafiti zimejuza hayo hivi karibuni.

Utafiti uliofanywa na Tanzania HIV/AIDS and Malaria Indicator Survey(THMIS) wa mwaka 2011-2012 kwa kushirikiana na  Taasisi ya Takwimu nchini(NBS) umegundua kuwa asilimia 59 ya kaya nchini zina uhakika wa kupata maji safi na salam, ambapo asilimia 44 ya kaya zinatumia zaidi ya dakika 30 kupata huduma maji.

Tanzania ni miongoni mwa nchini zilizosaini  mkataba wa Umoja wa Taifa wa mwaka 2002 kuhusu   Malengo ya Milenia   ikiwemo kuwapatia wananchi kupata maji safi na salama kwa asilimain 100  ifikapo mwaka 2025.

No comments:

Post a Comment