Tuesday, April 1, 2014

Watu milioni nane hufa kila kutokana na magonjwa yasiyoyakuambukiza

IMEELEZWA kuwa watu wapatao milioni nane wanakufa kila mwaka katika nchini zinazoendelea kutokana na magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Dr Julieth Shine ameeleza hayo mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembeyanga , Temeke jijini  Dar es salaam wakati wakihitimisha wiki ya upimaji wa hiari kwa magonjwa yasiyo yakuambukiza.

Dr Julieth ameeleza kuwa, magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na kisukari, saratani za aina zote, figo, kifua sugu, mishipa ya moyo na mishipa ya damu.
Amefafanua kuwa watanzania wengi hawana utamduni wa kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza hivyo wizara ya afya kupitia mfuko wa afya wa Taifa( CHF) na mfuko wa bima ya afya nchini (NHIF) uliamua kuendesha zoezi hilo la upimaji wa magonjwa ya kisukari, figo , kifua sugu, saratani za aina zote, mishipa ya damu na mishipa ya moyo kwa muda wa siku tano katika viwanja hivyo baada ya kugundua kuwa asilimia 43 ya wateja wa mfuko wa Bima ya  Afya ya Jamii nchini wana wanaugua magonjwa hayo. 
Kwa upande wa kimataifa . Takwimu zanajuza kuwa watu wapatao milioni thelathini na tano duniani wanakufa kila mwaka kutokana na magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Katika Tamasha hilo wananchi walipatia elimu kuhusu afya ya mam na mtoto, magonjwa yasiyo ya kuambukiza na elimu ya hali lishe.

No comments:

Post a Comment