Wednesday, April 30, 2014

RAISI Kikwete atuma rambirambi kwa mkuu wa mkoa wa Singida kufuatia vifo kutokana na ajali ya barabarani



RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kufuatia vifo vya watu 19 wakiwemo Askari Polisi wanne  na Viongozi watatu wa Kijiji kufuatia ajali ya barabarani iliyosababishwa na basi lililokuwa likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam katika Barabara kuu ya Singida - Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam,ajali hiyo ilitokea usiku wa April 27mwaka huu katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida baada ya basi la Kampuni ya Sumry lenye Nambari ya Usajili T. 799 BTE aina ya Nissan kuwagonga watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo ambapo ajali nyingine ilikuwa imetokea wakiwa pamoja na Askari Polisi kutoa msaada katika ajali nyingine iliyokuwa imetokea katika eneo hilo ambapo mwendesha baiskeli aligongwa na lori na kufariki papo hapo.

Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao kutokana na ajali hiyo, na amewahakikishia wafiwa kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huo mkubwa.

No comments:

Post a Comment