Wednesday, April 30, 2014

WAKULIMA wadogo washauriwa kutembeleana ili kubadilishana uzoefu



WAKULIMA wadogo nchini wameshauriwa kuwa na tabia ya kutembeleana mara kwa mara kwa ajili ya  kubadilishana uzoefu na wakulima wenzao ili waweze kupata mbinu bora za kilimo.

Rai hiyo imetolewa na maafisa kilimo katika kijiji cha IBINGU wilaya kilosa mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kutembeleana wakulima wanaotekeleza Mradi wa mabadiliko ya tabia nchi,Kilimo na kupunguza umasikini katika vijiji vya mradi ambavyo ni Madudumizi,Ilakala,Ibingu na Ulaya Kibaoni
Afisa kilimo kutoka MVIWATA Bwana Amanzi Amanzi amesema lengo la ziara hiyo  ni kuwasaidia wakulima wabadilike na kulima kilimo bora  chenye kuleta tija kwa kuwa tayari wamefundishwa  mbinu ambazo haziharibu mazingira.

Kwa upande wake Afisa kilimo kutoka Mtandao wa kijamii wa kuhifadhi misitu MJUMITA Bwana Ernest Jerome amewataka wakulima kushirikiana katika shughuli za kilimo na ndio maana wameamua kufanya ziara ya mafunzo ili kufahamiana na kubadilishana ujuzi.

Ziara hiyo imeandaliwa na mtandao wa vikundi vidogo vya wakulima nchini MVIWATA kwa kushirikiana na Mtandao wa jamii wa  kuhifadhi misitu TANZANIA  MJUMITA.

No comments:

Post a Comment