Wednesday, April 30, 2014

Nchi za Afrika kusini,Uingereza na Canada zachangia zaidi ya asilimia 70 ya uwekezaji toka njeongoza



IMEELEZWA  kuwa nchi ya Afrika ya kusini, Uingereza na Canada zilichangia kwa wastani wa zaidi ya asilimia 70 ya uwekezaji wote kutoka nje kati ya mwaka 2008 na 2011.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es salaam na wataalamu wa Benki kuu(BOT) Kitengo cha sera katika mahojiano maalum na mbiu ya maendeleo.

Wameeleza kuwa, Ripoti ya uwekezaji ya mwaka 2012 utafiti uliofanywa na Benki kuu,  , Taasisi ya takwimu nchini (NBS)  kuhusu hali ya uwekezaji nchini ilibaini kuwa nchi hizo ndizo zilizowekeza mitaji toka nchi kwa asilimia kubwa.

Wamesema, kilimo ambacho kina mchango mkubwa kwenye pato la taifa kiliendelea kuwa na kiwango kidogo cha uwekezaji toka nje ikilinganishwa na uwekezaji kkwenye shughuli nyingine kama uchimbaji wa madini na mawe, uzalishaji viwandani, fedha na bima  na habari na mawasiliano.
Mbali na hayo wamesema kuwa faida baada ya kulipa kodi iliongezeka kwa wastani wa asilimia 79.3 kila mwaka toka mwaka 2009 mpaka mwaka 2011

No comments:

Post a Comment