TUKIWA katika wiki ya malaria duniani takwimu toka viashiria vya ukimwi na malaria nchini inajuza kuwa miongoni mwa kaya zote nchini Tanzania,asilimia 95 ya kaya inatumia chandarua cha kuzuia mbu anayeeneza ugonjwa wa malaria ambapo asilimia 91 ya kaya nchini wana
tumia vyandarua vyenye dawa ya kuuwa mbu.
Taarifa toka wizara ya afya
na wadau wa Ukimwi na amalaria kwa vyombo vya habari zinaeleza kuwa hali hiyo
imetokana na wizara ya Afya na wadau mbalimbali wa mapmbano dhidi ya malaria
kugawa dawa , vyandarua na kutoa elimu ya afya kwa umma katika kila kona ya
Tanzania na kutumia vyombo mbalimbali vya habari katika kuelimisha jamii .
Umiliki wa vyandarua
katika kaya kwa asilimia tajwa hapo juu ni kiashiria tosha cha mafanikio ya
vita ya kupambana na ugonjwa wa malaria
.
No comments:
Post a Comment