Thursday, May 1, 2014

SERIKALI yaahidi kusimamia kusimamia matatizo ya wafanyakazi na kudhibiti mianya ya misamaha ya kodi



SERIKALI imesema itahakikisha inasimamia na kutatua matatizo ya wafanyakazi pamoja na kudhibiti mianya ya uingizwaji holela  wa bidhaa za nje ya nchi ambazo zinachangia kudidimiza soko la ndani.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Morogoro Bwana Said Amanzi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr.Joel Nkaya
Bendera katika kilele cha maadhimisho ya  sikukuu  ya wafanyakazi duniani iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro.

Bwana Amanzi ameyasema hayo wakati akijibu risala ya wafanyakazi iliyokuwa  ikiiomba serikali kudhibiti  bidhaa za nje kuingia nchini ili kutoa nafasi kwa soko la ndani.

Awali akisoma risala  ya wafanyakazi mratibu wa sherehe hizo Charles Luvunzo amewata wafanyakazi kuungana  ili kupatiwa mahitaji muhimu ikiwemo kupigania stahiki zao kwa kuhifadhiwa fedha katika mifuko ya jamii.

No comments:

Post a Comment