SERIKALI imeshauriwa kusaidia kutengeneza
miundombinu rafiki katika maeneo mbalimbali ikiwemo shuleni,itakayowawezesha
watoto wenye ulemavu kupata elimu kwa urahisi .
Aidha
imeshauriwa kuhakikisha inatekeleza sera ya Taifa inayoelekeza elimu bure kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa kujumuisha pia watoto wenye ulemavu.
Ushauri
huo umetolewa na Meneja Programu ya Elimu kutoka Shirika lisilo la
kiserikali la CCBRT linalotoa huduma kwa Watu wenye ulemavu, wakati wa
ziara ya wanahabari kwenye Kituo cha watoto wenye ulemavu kilichopo Manzese
wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam, ambapo tangu mradi wa kusaidia watoto
mashuleni uanze mwaka 2005 zaidi ya watoto 2000 wamenufaika, ingawa tatizo
kubwa ni kutokuwepo kwa mazingira rafiki kwa watoto hao.
No comments:
Post a Comment