Thursday, May 1, 2014

JIJI la Dar es salaam linatumia magunia elfu sitini ya mkaa kwa siku



ZAIDI ya hekari 400 za  mashamba ya miti zinateketezwa kila mwaka kwaajili ya kutengeneza mkaa, Imeelezwa.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya nchi toka mamlaka ya hali ya hewa nchini Dk Ladislaus Chang’a wakati akiongea na wanahabari kuhusu mabadiliko ya hali ya nchi na athari zake.

Dk Chang’a amefafanua kuwa viashiria vya madbadiliko ya hali ya hewa nchini ni pamoja na mafuriko kila sehemu kutokana na mvua chache zinazoendelea kunyesha,ongezeko la joto,mabadiliko ya msimu wa mvua,kuyeyuka kwa barafu mlima wa Kilimanjaro na ongezeko la ugonjwa wa malaria hata katika mikoa ambayo miaka ya nyuma ugonjwa huo halikuwa tishio.

Amesema mkoa wa Dar es salaam pekee huwa yanatumika magunia sitini elfu  ya mkaa kwa siku kwaajili ya matumizi mbalimbali.
.

No comments:

Post a Comment