WAZIRI wa
kazi na ajira Mheshimiwa Gaudensia Kabaka amesema pamoja na mabaraza ya kazi
kuangalia na kusimamia haki za wafanyakazi ni vema pia yakaangalia tija ya mfanyakazi
katika eneo lake la kazi ili kwenda sambasamba na madai yao.
Waziri
Kabaka ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
pili wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambapo amesema wizara yake
imejipanga kuimarisha na kuboresha ofisi za kazi mikoani kwa kuziongezea
bajeti mwaka huu jambo litakalosaidia katika kuboresha utendaji kazi
ikiwemo kuwafikia wafanyakazi walio pembezoni.
Waziri
Kabaka amesema mara nyingi kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hususani
wa sekta binafsi ambao wamekuwa hawaangalii utendaji wao kama unamnufaisha pia
mwajiri hivyo kuibua migogoro sehemu za kazi.
Aidha
ameyataka makampuni yote yanayojiuhusisha na uwakala wa huduma za ajira nchi
kujisajili ili kubaini yale yanayoendesha shughuli hizo kinyume cha sheria
ambapo amebainisha kuwa katika sheria za kazi zilizopo sasa hakuna suala la
kibarua katika maeneo ya kazi bali kuna mkataba wa muda mfupi, mrefu na wa
kudumu.
No comments:
Post a Comment