WAUMINI wa
kanisa la wa Adventista wasabato wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro,wamewataka wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuweka itikadi
zao za kisiasa pembeni pindi watakapo rejea Bungeni mjini Dodoma, ili
kuweza kupata katiba mpya itakayokidhi matakwa ya Watanzania ,badala ya
kuendeleza malumbano yasiyo na maslahi kwa Taifa .
Waumini
hao wametoakauli hiyo jana baada ya ibada maalumu ya kuwaombea vijana wa kanisa
hilo, walio hitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada , katika chuo
cha ualimu Greenbird kilichopo wilayani Mwanga mkoani humo.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti baadhi ya waumini wamesema, wamesikitishwa na
malumbano na kejeli zilizokuwa zikifanywa na baadhi ya
wajumbe wa bunge la katiba mjini Dodoma , hivyo wabadilike na
watumie muda uliobakia kurejesha busara zao kwa kukaa pamoja, ili
ipatikane katiba bora kwa manufaa ya Taifa.
No comments:
Post a Comment