BAADHI ya Wananchi wa
Mkoa wa Ruvuma wameisifu Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kuweza kusimamia
safari za Mabasi na kufanikisha kupanga safari katika sehemu ambazo zilikuwa na
kero ya usafiri kwa Wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza kwa niaba ya
Wasafiri wenzake katika Kituo Kikuu cha Mabasi Songea mapema leo ,mmoja ya
wakazi wa mji wa Songea Bwana Mohamedi Chichi,amesema katika Changamoto
zilizokuwa zinawakabili Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ni kukosa Usafiri wa Songea
– Dodoma, Songea – Mwanza na Songea – Mbamba Bay ambapo kwa sasa Njia
zote hizo zimefunguka na ameishukuru Serikali kwa kuweza kutatua changamoto
hiyo.
Nae Afisa Mfawidhi wa
SUMATRA Mkoa wa Ruvuma bwana Denis Daudi amesema Mkoa wa
Ruvuma una changamoto nyingi za usafiri, ikiwemo usafiri wa Songea – Mkenda
–njia ambayo inaunganisha Nchi ya Msumbiji na Tanzania pamoja na ile ya
Songea Tunduru ambayo bado inahitaji Usafiri wa uhakika.
No comments:
Post a Comment