Wednesday, April 16, 2014

ZAIDI ya kaya 424 Manispaa ya Morogoro zimeathirika na mafuriko



ZAIDI ya kaya 424 zilizopo Manispaa ya Morogoro zenye jumla ya watu 2120 zimeathirika na mafuriko hayo na  zinahitaji msaada wa kibinaadamu ambapo tayari  mifuko 200 ya unga wa sembe imekabidhwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya Morogoro kutoka ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini,mheshimiwa Abdul azizi Mohamed Abood yenye thamani ya shilingi milioni 4 na laki 6 kwa ajili ya  waathirika wa mafuriko yanayosababishwa na mvua hizo

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Joel Bendera amewataka wananchi waliojenga katika mikondo ya maji kuondoka mara moja ili kuepuka madhara yanayotokana na mafuriko.

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ilipotembelea na kuangalia maeneo ya Manispaa ya Morogoro yaliyoathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini


Dkt Bendera amesema, Serikali ya mkoa wa Morogoro inaendelea kufanya tathimini ya watu walioathirika na mafuriko ili iweze kuangali namna ya kuwasaidia.






No comments:

Post a Comment