WAKAZI WA Tarafa ya Kazimzumbwi, wilaya ya Kisarawe wameipongeza Halmashauri ya wilaya kwa kuendekleza na ukarabati wa barabara ya Kisarawe Mzenga na Kisarawe Maneromango kufuatila kuharibika kutokana mvua zinazoendelea nchini.
Wakiongea na mbiu ya maendeleo mapema leo katika kiji ji cha Kazimzumbwi wilayani humo , wananchi hao wamesdema kwasasa kuna unafuu wa usafiri baada ya Halmashauri kuanza ukarabati wa barabara hiyo kwani kwa takribani siku tatu hali ya barabara ilikuwa mbaya kiasi cha kusababisha usafiri wa kwenda Mzenga na Maneromango kupitika kwa tabu sana .
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wakandarasi wakikarabati eneo korofi ambalo linaanzia mwanzo wa msitu wa hifadhi wa Taifa wa kazi Mzumbwi.
Maeneo korofi katika njia hiyo ni Kisanga na Sungwi ambapo maji yamesambaa barabarani na kuhatarisha usalama wa abiria na magari.
No comments:
Post a Comment