Sunday, April 20, 2014

WANANCHI waipongeza Hospitali ya jeshi ya Lugalo jiini Dar es salaam.

WANANCHI jijini Dar es salaam wameipongeza Hospitali ya jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufunga maonesho ya Muungano kwa kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali  hali iliyosaidia wananchi wengi waliojitokeza kupima  kufahamu afya zao.

Wakiongea na mbiu ya maendeleo jijini Dar es salaam mapema leo, baadhi ya wananchi walisema, kitendo cha hospitali hiyo ya JWTZ kimeonesha ni kiasi gani n watu wengi wana utayari wa kupima afya zao lakini kukosekana kwa elimu ya kutosha na umaskini ni vikwazo katika kutekeleza jambo hilo.

Hospitali ya Lugalo iliendesha upimaji wa magonjwa ya sukari, shinikizo la damu , vvu sanjari na utoaji wa damu kwa hiari kwa wananchi mbalimbali waliotembelea banda la Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa , hasa idara  afya.

Wananchi waliweza kupata majibu ya vipimo mbalimbali na upimaji ulifanyika bila ya malipo.

No comments:

Post a Comment