Sunday, April 20, 2014

SERIKALI na wadau wa kilimo wahimizwa kuwekeza katika matumizi ya zana za kisasa za kilimo

SERIKALI na wadau mbalimbali wa kilimo wamehimizwa kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa kuwawezesha wakulima kielmu na kimitaji ili waweze kutumia zana za kisasa za kilimo kwa lengo la kujikomboa kiuchumi na kuleta mabadiliko katika jamii.

Meneja mauzo wa kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa zana za kisasa za kilimo yenye makao yake makuu Uingereza Bwana  Geoff Freed ameyasema hayo hivi karibuni jijini Dar  es salaam katika mahojiano maalum na mbiu ya maendeleo.

Amesema,matumizi ya zana za kisasa katika  sekta ya kilimo ndio mbdala sahihi wa kumkomboa mkulima mdogo, wakati na mkubwa kwani nchi zote zenye nia ya kweli ya kufanya mapinduzi ya kijani ni lazima zihakikishe wananchi wake wanapatiwa zana bora na za kisasa.

No comments:

Post a Comment