SERIKALI imeombwa kuwashughulikia watendaji Halmashauri wanaokula fedha zinazotengwa kwajili ya mapambano ya ukimwi katika Halmashauri mbalimbali za wilaya hapa nchini.
Wakiongea na wanahabari hivi karibuni , wananchi wa Mkuranga , mkoani Pwani wamesema kuwa, baadhi ya watendaji wa Halmashauri hasa wale wa kamati za ukimwi za wilaya wamekuwa wakifanya ufisadi fedha zainazotolewa na serikali na wahisani kwaajili ya mapambano dhidi ya ukimwi katika ngazi ya wilaya.
Ripoti za hivi karibuni toka ofisi ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali zinaonesha kuwa kasi ya kuliwa kwa fedha zinaotengwa kwaajili ya mapambano dhidi ya ukimwi zimefiki shilingi milioni 600,kwa Halamshauri hali inayoonesha kutofikiwa kwa mipango mikakati inayoweka na wafadhili na wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Taasisi ya kupambana na ukimwi nchini ( TACAIDS) ina mkakati mkubwa wa sifuri tatu ambao unalengo la kutokeza maambukizi ya ukimwi nchini. Je kwa hali hii mpango mkakati huu utafanikiwa?Wamehoji wananchi hao.
No comments:
Post a Comment