ZOEZI la uandikishaji wa
vitambulisho vya mkazi bado linaendelea jijini Dar es salaam kwa wale
wasiojiandikisha, hivyo wananchi ambao bado hawajajiandikisha wamehimizwa
kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata vitambulisho.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na hifadhi hati wa mamlaka ya
vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA)Bwana Thomas William ameyasema hayo hivi
karibuni katika mahojiano na mbiu ya maendeleo.
Amesema kuwa wameamua kuendelea na zoezi hilo kwakuwa imebaini watu wengi hawajajiandikisha na kumekuwa na
ongezeko la watu wengi kuhamia katika jiji la Dar es salaam ni vyema zoezi hilo
likachukua muda mrefu.
Amesema lengo la vitambulisho ni kutofautisha kati ya watanzania
na wasio watanzania.
No comments:
Post a Comment