MBUNGE wa Jimbo la Songea
mjini Mheshimiwa Dokta Emanuel Nchimbi amewataka wananchi wa Manispaa ya
Songea kuwa na tabia ya kuchukia Uchafu na kubuni mbinu mbalimbali za
kukabiliana na ongezeko la Taka kwa kusimamia sheria walizo jiwekea.
Dokta Nchimbi ameyasema hayo jana wakati akikabidhi magari
matatu mawili makubwa kwa ajili ya kuzolea taka na Moja dogo kwa ajili ya
matumizi ya Manispaa ya Songea yakiwa yame gharimu kiasi cha shilingi milioni
478.9.
Amesema msaada wa Magari hayo umetokana na juhudi za
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
kusimamia maombi ya ufadhili kutoka Benki ya Dunia akishirikiana na
uongozi wa Mkoa wa Ruvuma.
Aidha mbunge huyo amesema kuwa pamoja na mradi wa
magari kukamilika suala la kuboresha miundombinu ya Maji tayari limepatiwa
ufumbuzi kwa kutengewa bilioni moja katika bajeti ijayo, sanjari na mradi
wa ujenzi wa barabara yenye umbali wa kilometa 15.
No comments:
Post a Comment