Monday, April 21, 2014

SERIKALI yaombwa kuweka jitihada katika kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama



WANANCHI wa kijiji cha kiegeya kata ya Berega wilaya ya kilosa Mkoani Morogoro,wameiomba serikali kuweka jitihada  katika kuhakikisha wanaondokana na tatizo la ukosefu wa  maji safi na salama.
                       
Wakizungumza  kwa nyakati tofauti  na Mbiu ya maendeleo,hivi karibuni,wamesema kuwa tatizo la maji limekuwa la muda mrefu na kwamba waliitikia wito wa serikali katika kuchangi ili kuweza kupata huduma hiyo jambo ambalo limekuwa halileti majibu ya uhakika.

Aidha Wamesema kuwa huamka saa nane za usiku kuwahi maji na hutembea umbali wa kilomita tano jambo linalowafanya washindwe kufanya shughuli za maendeleo, ambapo ndoo moja ya maji uuzwa kati ya shilingi 700 na 1000

Nae  Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana John Lucas  amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la maji ambapo amesema kuwa kwa sasa wana mpango wa kufadhiliwa na shirika moja kutoka umoja wa makanisa duniani lijulikalo kama Trufood ambalo litawajengea bwawa la kuhifadhia maji.


No comments:

Post a Comment