WANANCHI wa vijiji 57 vya wilaya ya Kondoa Mkoani
Dodoma, wamehimizwa kutumia fursa iliyojitokeza ya kupata umeme katika maeneo
yao, ili waweze kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wao.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katika kijiji cha Itololo,
wilayani Kondoa, wakati alipokuwa akikagua utekelezaji wa mradi wa umeme
vijijini,ambapo kwa mkoa wa Dodoma utagharimu shilingi bilioni 43.9.
Naye, Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Bi Zabein
Mhita akizungumza kwa niaba ya wananchi wa vijiji vitakavyofikiwa na mradi huo
wa umeme, amesema mwamko ni mkubwa kutoka kwa wananchi hao, kwa kuwa wanatambua
umuhimu wa umeme katika maendeleo yao.
Hatua iliyofikiwa kwa sasa ni upelekaji wa
nguzo za usimikaji wa umeme katika vijiji hivyo, na inatarajiwa kuwa pindi
umeme huo utakapowashwa utasaidia kuongeza thamani ya mazao ya wananchi wa
vijiji hivyo kwa kuyasindika, na hata huduma za jamii kama shule na hospitali,
kuwa bora zaidi.
No comments:
Post a Comment