KAMATI ya Fedha na uongozi ya
manispaa ya Morogoro imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo hospitali ya wilaya ambayo imeanza kujengwa katika kata ya Mkundi
Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika
jana Meya wa Manispaa ya Morogoro bwana Amir Nondo amesema ujenzi huo umefikia
hatua nzuri na wanasubiri kapata fedha awamu ya pili ili waweze kukamilisha
jengo hilo ambapo ameishukuru serikali kwa kuwapatia fedha.
Bwana Nondo amefafanua kuwa wamejenga hospitali
hiyo ya wilaya katika kata ya Mkundi kutokana na wakazi wa kihonda, Mkundi na
maeneo mengine kuwa mbali na huduma ya afya.
Ujenzi wa hospitali hiyo unaotarajia kukamilika
April 26 mwaka huu hadi sasa umegharimu kiasi cha shilingi milioni mia tano na
elfu themanini na tano.
No comments:
Post a Comment