Saturday, May 17, 2014

TUME ya kurekebisha sheria nchini yakabidhi taarifa ya mapitio ya migogoro ya ardhi nchini



TUME ya kurekebisha sheria nchini, imekabidhi taarifa ya mapitio ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya aridhi nchini, kwa waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro.

Akikabidhi taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Nchini Jaji Aloysius Mujuluzi, amesema tume yake imeonelea kuangalia eneo hilo ambalo limekuwa linalalamikiwa  na wananchi, ili kutoa mapendekezo ya namna sheria hiyo inavyoweza kurekebishwa, kuondoa kasoro za kisheria na kutekelezwa kwa ubora na mafanikio zaidi.

Akipokea taarifa hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Migiro amepongeza juhudi zinazofanywa na tume kuhakikisha sheria zina kwenda na wakati, na zile zenye kasoro zinarekebishwa, na hivyo ameahidi wizara yake kuchukua kwa uzito unaostahili mapendekezo yaliyotolewa,ambapo akatoa rai kwa watendaji.

Mapitio ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya aridhi, yanafanywa baada ya miaka kumi toka mfumo huo uanzishwe nchini, kupitia mahakama maalum za ardhi, ili kuona na kupima ufanisi wa taasisi hizo juu ya dhamana kubwa ya kutatua migogoro ya ardhi, huku ikizingatiwa kuwa aridhi ndio msingi wa maisha ya mwanadamu.





No comments:

Post a Comment