WATANZANIA wamekumbushwa kutambua umuhimu wa kutunza na
kuhifadhi mazingira ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kutopoteza wanyama
kwa kuwa ni miongoni mwa rasilimali zinazoliingizia taifa mapato kwa kiasi
kikubwa.
Akizunguma
na baadhi ya Walimu wa Shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es salaam, ambao
walikuwa wakipatiwa elimu juu ya kuwawezesha vijana mashuleni kujua faida za
utalii, uhifadhi wa mzingira na kutambua fursa zilizopo katika sekta ya utalii,
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii
Bw. HERMAN KARARYO, amesema licha ya mabadiliko ya Tabia nchi kuleta matatizo,
lakini wananchi wenyewe wamekuwa wakisababisha uharibifu wa mazingira.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanawake , Vijana na Mazingira
AWEIDA Halima Mamuya amebainisha kuwa wakati umefika sasa wa kuwawezesha
wanafunzi mashuleni kutambua umuhimu wa kutunza, kuhifadhi na kujua fursa za
utalii tangu wakiwa wadogo.
Mkutano
huo umeandaliwa na Chama cha Maendeleo ya Wanawake , Vijana na Mazingira AWEIDA
kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri na Utalii Afrika Mashariki
GTTP.
--------------------------------------------------------------------------------
No comments:
Post a Comment