WALIOKUWA
wanachama wa chama cha kupanda na kuvuna DECI Wilayani Kilosa wameiomba serikali
iwarejeshee pesa zao kama ilivyowaahidi au itoe tamko lolote juu ya pesa zao
ili wafahamu kinachoendelea.
Wakizungumza na Mwandishi wa Habari
Kilosa baadhi ya wanachama hao wamesema serikali imekaa kimya kwa muda
mrefu kitu ambacho kinawapa wasiwasi wa kurejeshewa pesa zao kama serikali
ilivyowaahidi.
Mmoja wa wanachama hao Nassoro
Machengo ambaye alipanda zaidi ya milioni moja amesema baada ya serikali
kuthibitisha na kuifungia Taasisi hiyo na kuipeleka mahakamani ili ahidi kurejesha
pesa kwa wananchi waliotoa fedha zao DECI wenye ushahidi wa vielelezo mara tu
kesi hiyo itakapokamilika .
Ni miaka 7 sasa tangu Taasisi ya
kifedha ya DECI iliyokuwa ikijiendesha katika utaratibu wa kupanda na kuvuna
pesa ambapo wananchi mbalimbali waliwekeza pesa kwa lengo la kuvuna pesa
zaidi , lakini Taasisi hiyo ilikuwa ikiendeshwa kinyume na taratibu za kisheria
hivyo serikali ilisimamisha kufanya shughuli hizo huku ikiwa imekusanya
mabilioni ya watanzania.
No comments:
Post a Comment