CHAMA cha Watu wenye ulemavu Mkoa wa Mara
CHAWATA kimeiomba Serikali kushirikishwa katika Masuala mbalimbali yanayowahusu
ikiwemo kujengewa uwezo ili kujitegemea na kuondoa dhana ya watu wenye ulemavu
ni tegemezi.
Wakiongea
katika Jukwaa la Majadiliano kuhusu ujumuishwaji na utetezi wa Mahitaji na haki
za watu wenye ulemavu wa viungo, baadhi ya watu wenye ulemavu mkoani Mara
wamesema kuwa wamekuwa wakitengwa katika mambo mbalimbali ikiwemo kutokuwepo
kwa miundombinu rafiki katika baadhi ya ofisi mkoani humo na kuwa kikwazo
katika kupata huduma wanazozihitaji.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CHAWATA Mkoa wa Mara Bw Yohana Magai amesema kuwa ni
vigumu masuala ya watu wenye ulemavu kujadiliwa na watu wasiokuwa na ulemavu .
CHAWATA
mkoa wa Mara kimeweza kufanya Majadiliano hayo katika Jukwaa hilo kwa ufadhili
wa Taasisi ya The foundation For Civil Society ya jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment