Sunday, May 18, 2014

WIZARA ya Maliasili na Utalii imeshajiishwa kuweka mazingira mazuri kwa watalii wa ndani


  
WIZARA ya Utalii nchini, imeombwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha watalii wa ndani kutembelea vivutio vilivyopo nchini  bila kupitia katika makampuni ya kupandisha watalii na badala yake waruhusu vikundi binafsi ili kuleta muamko kwa  watanzania wengi kuvitembelea vivutio hivyo.

Wakiongea baada ya kutembelea uwanda wa kilele cha mshira katika mlima Kilimanjaro,hivi karibuni baadhi ya watalii wa ndani wamesema, watanzania hawana utamaduni wa kuvitebele vivutio vya nchi yao kutokana na kukosekana kwa hamasa, pia urasimu wa kuvitembele vivutio hivyo.

Wamesema ili kuleta muamko kwa watanzania ,wanaiomba wizara husika kuweka viwango ambavyo        wananchi wa hali ya chini wanaweza kuvimudu, pia kutoa elimu na hamasa kuanzia shule za msingi ili jamii iweze kujengwa katika misingi ya kuvitambua na kuvithamini vivutio vyao.

No comments:

Post a Comment