HALMASHAURI ya manispaa ya Morogoro imeaanza
zoezi la kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa lengo likiwa ni kutokomeza
ugonjwa huo.
Afisa
mifugo wa kata ya Kichangani Bi Mary Shayo amesema chanjo hiyo inatolewa kwa
mwaka mara moja na kuwahamasisha wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi
kwenye zoezi hilo.
Aidha
bi Shayo amesema kuwa malengo yao ni kuchanja mbwa wapatao mia mbili hivyo
wananchi wanatakiwa kutambua umuhimu wa kupeleka mbwa pamoja na paka ili waweze
kupatiwa chanjo hiyo.
Tatizo
la ugonjwa wa kichaa cha mbwa linaongezeka siku hadi siku hivyo elimu zaidi
inatakiwa kutolewa kwa wananachi ili kupunguza tatizo la ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment