Monday, May 19, 2014

MAKTABA ya wilaya ya Kilosa inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo



MAKTABA ya wilaya ya Kilosa ,mkoani Morogoro inakabiliwa na changamoto mbalimbali hali inayopelekea maktaba hiyo kushindwa kujiendesha vizuri.

Hayo yameelezwa jana na mkutubi wa maktaba hiyo James Mgunga wakati akiongea na mwandishi wetu ofisi kwake na kuzitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uchakavu wa jengo la maktaba,upungufu wa vitabu vya kiada na uhaba wa wasomaji.

Mgunga amesema kuwa changamoto hizo zinapelekea wasomaji kushindwa kujtokeza kwa wingi kwenda kujisomea katika maktaba hiyo  hali inayochangia maktaba hiyo kushindwa kujiendesha kwani inategemea mapato kutoka kwa wasomaji.
Kutokana na hali hiyo mkutubi huyo amewaomba wafadhili na wadau mbalimbali wa maendeleo wajitokeze kukarabati  jengo la maktaba ili liwe katika hali nzuri kwani iliyopo sasa ni mbaya kwani  jengo limechakaa sana.

No comments:

Post a Comment