WADAU
wa kahawa mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya tathimini ya kina kuhusu
matatizo yanayo kikabili kilimo cha zao la kahawa ,kisha kuyatafutia ufumbuzi
ili zao hilo liweze kulimwa kwa wingi na mkoa huo uweze kukuza uchumi wake na Taifa
kwa ujumla
Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Leonidas Gama, wakati akifungua
warsha ya wadau wa kilimo cha zao la kahawa iliyofanyika mjini Moshi,
ambapo amesema mkoa huo uko nyuma kiuchumi ,kutokana na baadhi ya wakulima
kubadili kilimo cha kahawa ,na kuanza kulima mazao ya aina
nyingine.
Bw Gama
amezitaja sababu za kushuka kwa kilimo hicho,ni pamoja na wakulima
kutozingatia kanuni za kilimo bora ,ufinyu wa ardhi kutokana na ongezeko
kubwa la idadi ya watu , vijana kukimbilia mijini na kuwaachia wazee shughuli
za kilimo ,pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya
wakulima wa kahawa waliohudhuria katika semina hiyo ,wameiomba serikali
iwapatie wakulima hususani vijana elimu ya kilimo bora pamoja na pembejeo
,ili vijana hao wasikimblie mijini na kuwaachia wazee kazi za mashambani
No comments:
Post a Comment