WAFANYABIASHARA wa maduka ya jumla na rejareja wilayani Kilosa wametakiwa
kucha tabia ya kuanika juani biashara za vyakula ili kuepuka madhara ya kiafya.
Wito huo umetolewa na afisa afya upande
wa chakula na vipodozi[TFDA]wilayani Kilosa Bwana Fransis Jacob ofisini kwake mapema leo wakati akiongea na wanahabari kuhusu majukumu na kazi za mamlaka ya chakula na
madawa nchini(TFDA)
Jacob amesema kuanika bidhaa juani
kunaharakisha bidhaa kuisha muda wake hivyo amewataka wauzaji wa bidhaa kuacha
tabia hiyo.
Amesema lengo la mamlaka ya chakula
dawa na vipodozi TFDA ni kulinda afya ya wananchi na jamii kwa ujumla kwa
kuzuia athari ambazo zinaweza kujitokeza
kwa mlaji.
No comments:
Post a Comment