SERIKALI imesema inaendelea na
ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara hadi Mlimba wilayani Kilombero mkoani
Morogoro ili barabara hizo ziweza kupitika kwa muda wote ambapo kwa
sasa zinafanyiwa upembuzi yakinifu ili kuweza kuanza
ujenzi wake mara moja.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu waziri wa Ujenzi
mhandisi Gerson Lwenge alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Abdul
Mteketa aliyetaka kujua ni lini barabara za jimbo lake zitakamilika kujengwa
ili ziweze kupitika kwa mwaka mzima kuliko ilivyo hivi sasa ambapo
barabara nyingi hazipitiki na kupelekea adha kwa wakazi wa eneo hilo
Wakati
huohuo Serikali imetupiwa lawama kwa kushindwa kusimamia elimu nchini na badala
yake serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi inasaidia
kuididimiza elimu kutokana na mipango yake isiyo zingatia taaluma na
umakini kama ilivyojitokeza kwenye ufaulu wa mitihani ya kidato cha
nne mwaka jana kwa kuwa na sifuri nyingi na kuongeza madaraja ya
ufaulu yasio kuwa na tija.
Lawama
hizo zimetolewa na msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mheshimiwa Suzan
Limo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo na kusema, serikali inakwepa
wajibu wake katika kuendeleza elimu nchini badala yake inasaidia kushusha elimu
kwa kutowajibika ipasavyo
No comments:
Post a Comment