WANANCHI wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameiomba wizara ya
afya na ustawi jamii kupitia wataalamu wa Afya wa halmashauri kuaandaa mpango
maalum wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa wa homa ya Dengue.
Wakiongea na wanahabari mjini Ifakara mapema jana ,wananchi
hao wamesema kuwa, watu wengi hawana ufahamu wa kutosha juu ya ugonjwa wa
dengue hivyo ni vyema serikali ikachukua tahadahri kwa kuhakikisha kuwa
wananchi wanapatiwa elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo.
Mazingira ya Ifakara yanafanana na yale ya
jiji la Dar es salaam, hivyo huenda ugonjwa huo ukaingia wilayani kwetu,
sasa wizara ni lazima ihakikishe inatuapatia wananchi wake elimu ya kutosha ,
walisema wakzi hao wa Ifakara , Kilombero
No comments:
Post a Comment