Friday, May 30, 2014

WIZARA ya Nishati na Madini yakanusha madai ya wabunge wa upinzani kuhusu makampuni kukwepa kodi



SERIKALI imekanusha madai yanayotolewa na baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa  Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya mkoani Shinyanga haijalipa kodi toka mwaka 1947.

Naibu Waziri wa Nishati   na Madini Setven Juliasi Masele amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akihitimisha makadirio ya wizara yak e kufuatia tuhuma mbalimbali za ukwepaji wa kodi zinazofanywa na baadhi yab makampuni ya uchimbaji hapa nchini  toka kwa wabunge wa upinzani.

Amesema kuwa, Kampuni ya uchimbaji  wa dhahabu ya ya Mwadui ya mkoani Shinyanga toka ianzishwe mpaka sasa imelipa kodi ya shilingi bilioni 178 .

Amesema mbali na kulipa  kodi  serikali kuu , kampuni hiyo ya Mwadui imelipa kodi katikaHalmashauri ya Kahama kama shauri inavyoitaka kila uchimbaji wa  kampuni ya madini nchini kulipa ushuru  wa kiwango maalum katika Halmashauri husika  

No comments:

Post a Comment