Thursday, May 29, 2014

WAGANE wawezeshwa mikopo ili kukabiliana na changamoto za maisha



MPANGO wa kuwasaidia mikopo wanaume waliofiwa  na wake zao  (WAGANE) umeanza kufanyika katika kata za MBUMI  na KASIKI katika mamlaka ya mji mdogo wa  Kilosa,mkoani Morogoro. 
Akizungumza  mapema leo na Mbiu ya maendeleo  kwenye kata ya Mbumi Afisa maendeleo ya jamii wa kata hiyo Bi  Avintishi Abdallah  amesema kuwa mchakato huo umeanza ambapo kwenye kata hiyo wameshapokea wagane 8.

Bi Abdala ameeleza kuwa ili wagane hao waweze kunufaika na mkopo huo wanapaswa waunde  vikundi kwa watu wasiopungua (5)  huku akiwahimiza wagane waliopo  katika kata hiyo kujitokeza kwa  wingi ili waweze kufaidika na mikopo hiyo itakayosaidia kujiletea maendeleo na kuendelea kulea vyema familia zao.

No comments:

Post a Comment