HALMASHAURI ya
Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro imeshauriwa kutenga fedha za kutosha katika
Bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kumtuma
mkaguzi kukagua matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo zilizotumika kwenye miradi
wilayani humo.
Ushauri huo umetolewa mapema leo na
kamati za mifuko ya jimbo zilipokuwa zikifanya majumuisho ya ziara ya kukagua
miradi inayokarabatiwa kwa fedha za mifuko ya jimbo la Kilosa na Mikumi
Wilayani humo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya
Habari katibu wa mifuko ya jimbo Mtila Mbaruku amesema zaidi ya miradi 22
imekaguliwa ambapo jimbo la Kilosa kati miradi 14 na Mikumi ni miradi 8 na
kwamba baadhi ya miradi imejengwa chini ya kiwango kutokana na kamati za vijiji
kuwa na matumizi mabaya ya fedha.
Akizungumzia miradi iliyojengwa
chini ya kiwango , ameitaja kuwa ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika
shule ya msingi kitunduweta na mradi wa barabara ya Mabura Mafera
yenye urefu wa kilomita tano ambayo imekarabatiwa chini ya kiwango
hali iliyopelekea kusombwa na maji na kusababisha wananchi
kushindwa kusafiri kwa haraka wanapopatiwa matatizo.
Kutokana na hali hiyo Mtila
amewataka viongozi wa serikali za vijiji kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha
zote za serikali zinazopelekwa kwenye vijiji vyao kwa ajili ya maendeleo ya
wananchi.
No comments:
Post a Comment