KATIBU wa chama cha United Democratic Party UDP mkoa wa Morogoro
Ununi Mn’goo(61) amefariki dunia jana nyumbani kwake kijiji cha Kikundi baada
ya kuugua kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa UDP Mkoa
Dominick Ponela,Katibu huyo alikuwa akisumbuliwa na Maralia ya vipindi sambamba
na vidonda ndani ya kifuani.........
.Ponela
alisema tayari amewasiliana na makao jmakuu ya chama hicho jijini Dara es
salaam na ofisi imeahidi kushiriki mazishi hayo yanayotaraji kufanyika kijijini
hapo leo majira ya jioni.
Mng'oo ambae ni miongoni
mwa waasisi wa chama hicho Mkoani Morogoro na nchini pia aliwahi kuwa mwalimu
wa shule ya msingi,Mratibu elimu kata ya Tegetelo,Katibu wa utamaduni wilaya na
mwenyekiti wa asasi binafsi ya Tushikamane.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu marehemu alikuwa na wake wawili akiwemo aliyefunga nae ndoa ya dini,mwingine aliyefunga ndoa Bomani sambamba na watoto nane.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu marehemu alikuwa na wake wawili akiwemo aliyefunga nae ndoa ya dini,mwingine aliyefunga ndoa Bomani sambamba na watoto nane.
No comments:
Post a Comment