Thursday, May 29, 2014

SERIKALI Kilosa kudaiwa milioni 800 kwa kumvamia mwekezaji


BAADA ya Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kutoa idhi kwa wanakijiji cha Mbigili kitongoji cha Mateteni kugawana ardhi ya Mwekezaji Mees Estate Ltd kwa madai kuwa imefutiwa umiliki wake,uongozi uliowekeza katika ardhi hiyo umeibuka ukilaani vikali kitendo hicho na kudai fidia ya shingi Mil.800.

Mbele ya waandishi wa habari mjini Morogoro mmoja wa wakurugenzi wa Mees Estate Ltd inayomiliki mashamba ploti namba 28,29 na 32, Patrick Mees alisema chokochoko hizo dhidi ya mashamba hayo yenye ukubwa wa ekari 1,466 zimesababisha kushusha uzalishaji mwaka huu na kuamsha hofu dhidi ya uhai wao na mali shambani hapo.

“mashamba haya tunayamiki kihalali kwa hati ya umiliki ya 1987 na tangu kipindi hicho tunayatumia kuzalisha zaidi ya tani 25,000 za aina mbalimbali za nafaka ukiwemo Mpunga na Mahindi licha ya uwekezaji mwingine kama Majengo,mifugo,majosho na msitu wa miti ya Mbao aina ya Mkongo” alisema

 Juzi wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya Ardhi wilayani humo Anna Sanga,Afisa ardhi wilaya Arnold Selestine na Mwanasheria wilaya Ocate Maganiko walifika ktongoji cha mateteni na kuuagiza uongozi wa kijiji hicho kugawana mashamba ploti namba 28,29 na 32.

Kwa mujibu wa viongozi hao kijijini hapo,uamuzi wa halmashauri hiyo kugawa shamba hilo unatokana mashamba hayo kufutiwa umiliki wake na rais mwaka 2000 kisha kurejeshwa kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment