MKAZI wa Kijiji cha Mwembetogwa kata ya Muungano Wilaya ya Mtwara
vijijini,mkoani Mtwara Mohamed Chumila
amekutwa amefariki baada ya kusukumwa na mwanamke wa kijiji cha jirani alipoenda
nyumbani kwake usiku
.
Afisa mtendaji wa
kijiji hicho Nicolaus Mrope amesema mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umeanguka
nje ya nyumba ya mwanamke huyo na amekiri kumsukuma pasipo kujua kama
angekufa.
Mrope ameeleza kuwa
mwanamke huyo amedai kuwa marehemu alifika nyumbani kwake saa nne usiku na
kugonga mlango na alipofungua alikutana naye na kumtaka wafanye mapenzi na
alipomkatalia ndipo wakaanza kuvutana.
Ameeleza kuwa baada ya
kumsukuma alirudi ndani na kujifungia akiamini mwanaume huyo angeamka na kurudi kwa
mke wake, lakini alipoamka asubuhi alikuta umati wa watu nje ya nyumba yake
wakishuhudia maiti ya Chumila.
Mwanamke huyo bado
anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment