WIZARA ya Maliasili na Utalii imetakiwa
kuangalia sheria za ujirani mwema na vijiji jiarani na hifadhi za taifa kwa
kuhakikisha kuwa jamii inapata ushirikiano wa kutosha toka kwa wafanyakazi wa
idara ya maliasili hasa askari wa maliasili.
Changamoto hiyo imetolewa na wakazi wa vijiji vya Sanze na
Mangula vilivyopo wilayani Kkilombero, mkoani Morogoro kufuatia baadhi ya watumishi kutokuwa na ushirikiano mzuri na
wananchi wa vijiji hivyo.
Wakiongea na Mbiu ya maendeleo leo asubuhi katika kijiji cha
Sanze wilayani humo, baadhi ya wananchi wamesema kuwa, ni kweli maliasili ni
muhimu kwa maendeleo ya Taifa hasa katika kuingiza pato Taifa lakini ni vyema
wizara ikatambua kuwa kabla ya kuanzishwa kwa hifadhi hizo wananchi walikuwepo
na wanahaki ya kutumia baadhi ya rasilimali kwa kupata maelezo toka kwa wakuu
wa idara husika.
Wamesema , baadhi ya watendaji wa maliasili hawana uhusiano mzuri na wanakijiji
jambo ambalo linakwamisha uafanisi wa uendelezaji wa maliasili za Taifa kupitia
misitu ya Hifadhi za Taifa na wanyama pori.
Kufuatia hali hiyo wameiomba wizara ya maliasili kuwa na
semina ,warsha na makongamano ya mara kwa
mara katika vijiji jirani na hifadhi za taifa kwa lengo la kutoa elimu
kwa umma namna ya kutumia maliasili hizo sanjari na utii wa sheria na kanuni
zilizowekwa na wizara ya maliasili.
No comments:
Post a Comment