MAITI ya mtoto mchanga
imeokotwa ikiwa imevilingishwa kwenye kanga na
kuwekwa kwenye mfuko wa rambo imeokotwa ikiwa
imetupwa pembezoni mwa mto uliopo mabibo
External jijini dares-salaam.
Mwili wa mtoto huyo umegundulika na
muokota chupa za plastiki ambapo alitoa taarifa
polisi , ambapo askari polisi walifika
eneo la tukio na kukuta maiti hiyo.
Akizungumza na mbiu ya maendeleo, Askari wa jeshi la polisi , sajest primi
Joseph aliyeuchunguza mwili huo amesema hilo ni tukio la tatu mfululizo
kutokea katika mto huo na matukio mengine ya aina
hiyo yamepishana mwezi mmoja .
Mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wamelaani vikali kitendo hicho
na kusema wanadamu wamekuwa hawana utu na hivyo kufanya matendo
ya kinyama bila uoga .
Aidha wametoa lawama zaidi kwa madaktari ambao
wanawasaidia akina dada kutoa mimba na kuwataka kuacha
tabia hiyo
No comments:
Post a Comment