MWENYEKITI wa Jumuiya ya uchumi na maendeleo ya walemavu
nchini(JUMAWATA) Bwana Mshamu Mzanda amezitaka Taasisi na mashirika ya watu
binafsi nchini kujitokeza katika kijiji cha Mtamba wilayani Kisarawe kuwasaidia
walemavu wa kiislamu kuwajengea msikiti kwaajili ya kufanya ibada.
Akiongea na Mbiu ya Maendeleo
wilayani Kisarawe mkoani Pwani mapema leo, mwenyekiti huyo amesema kijiji cha Mtamba
wilayani humo kina walemavu 324 wenye
dini tofauti huku zaidi ya asilimia 50 ya walemavu hao wakiwa ni waislamu lakini hawana nyumba ya ibada.
Amefafanua kuwa, wakristo wana
kaniasa ambalo limejengwa kwa msaada wa Taasisi moja toka nchini Korea toka
hali ambayo inawafanya wamuabudu mwenyezimungu katika mazingira mazuri kinyume
na waislamu.
Amesema , wao hawahitaji fedha
wananchihitaji kujenga msikiti kwaajili ya ibada kisha wakabidhiwe kiongozi wa
dini na mwalimu kwaaajili ya kuwafundisha dini watoto wa kiislamui wa jamii ya walemavu.
JUMAWATA ina jumla ya ekari 450
iliyopewa na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani mnamo mwaka 2007
kwaajili ya kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji.
No comments:
Post a Comment