IMEELZWA kuwa
ujenzi wa Barabara ya Rudewa mpaka machimbo ya makaa ya m awe Mangaka ni
mkombozi wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii wilayani Rudewa na mkoani Njombe
kwa ujumla.
Wananchi wa vijiji vya Mlangali
wilaya ya Rudewa , mkoani Njombe
wameeleza hayo mwishoni mwa wiki wakati wakiongea na mbiu ya maendeleo katika
kueleza shukrani zao kwa serikali na wadau wa maendeleo waliofanikisha ujenzi
wa barabara hiyo ambayo inatarajiwa kuwa mkombozi wa ajira kwa wananchi hao.
Wamesema kuwa , kwa muda mrefu wilaya hiyo nyuma kimaendeleo
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uchakavu wa muda mrefu wa miundo mbinu ya
barabara inayounganisha wilaya hiyo na
mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Iringa.
Hata hivyo wananchi hao wameiomba
serikali kuhakikisha kuwa mgodi wa maka yam awe wilayani humo unatoakipaumbele cha ajira kwa wazawa
ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuondokana na umaskini wa
kipato.
No comments:
Post a Comment