Saturday, June 14, 2014

BARAZA la madiwani Mbarali laondoa tozo ya ushuru wa nafaka




 
Madiwani wakiomba dua kabla ya kuanza kikao

HATIMAE baraza la Madiwani halmashauri ya Mbarali mkoani Mbeya limetengua tozo ya ushuru wa shilingi 2000 kwa gunia la nafaka vijijini na kurejesha tozo la awali la shilingi 1000 baada ya mvutano wa muda mrefu kati yake na wakulima.


Mvutano huo uliomlazimu Mkuu wa Mkoa huo Abbas Kandoro kuagiza kuitishwa haraka baraza la dharula lililokutana Mei 27 ulitokana na wakulima kuhoji sababu ya kulipa tozo hilo wakati wao si wafanya biashara.
Akizungumza uamuzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Keneth Ndingo alisema Halmashauri inaingia kwenye tatizo lingine la kuziba pengo la hasara ya shuilingi Mil.640 litakalojitokeza baada ya kuondolewa kwa tozo hilo.

Hata hivyo aliongeza kuwa sambamba na kushushwa kwa tozo hilo pia Mawakala wa kukusanyaji ushuru huo watapungua kutoka kumi hadi wanne ili kuleta ufanisi na kurahisisha udhibiti wa mapato unaosababisha hati chafu ya ukaguzi.

Baadhi ya wakulima Christopher Uhagile na baadhi ya madiwani mbali na kupongeza juhudi za mkuu wa mkoa kwa kutatua tatizo hilo haraka walimlalamikia Mbunge wa Jimbo la Mbarali Modestus Kilufi kwa kupinga mabadiriko hayo

No comments:

Post a Comment