MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya,
imemwachia huru Andrea Shadrack Mwalimu wa shule ya sekondari ya
Montforty inayomilikiwa na kanisa la Katoliki Rujewa baada ya kuoenekana
hana hatia kutokana na kosa la kubaka lilokuwa linamkabili.
Shadrack ambaye ni
‘Bruda’ wa kanisa la Katoliki kigango cha Iringa alifikishwa mahakamani hapo
akidaiwa kutenda kosa hilo ndani ya shule hiyo Septemba 12 mwka jana saa
3:30 asubuhi.
Akitoa hukumu hiyo
Hakimu wa Mahakama hiyo Kinabo Minja, amesema Mahakama inamwachia huru
mshitakiwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha ushahidi wa
tukio hilo
Hakimu huyo
amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wa vielelezo
ikiwemo fomu namba tatu ya polisi (PF3) ambayo hutolewa kwa mlalamikaji ili
aweze kupatiwa matibabu kuonekana kuwa na utata.
.
No comments:
Post a Comment