Sunday, June 15, 2014

WANANCHI jijini Hongkhong,nchini China wadai ndoa si jambo muhimu katika maisha






TAFITI  za hivi karibuni zilizofanyika jijini  Hong khong ,nchini China zinaonesha  kupungua kwa watu wanaojihusiha na suala la ndoa kwani wamedai haina ulazima katika maisha ya binadamu.


Ripoti hiyo inafafanua kuwa Wanawake wengi  katika jiji la Hongkhong wanpenda kufurahi, kuzungumza na kukutna na marafiki zao huku wakifurahia utaratibu huo wa maisha,.
 Watu wengi zaidi katika jiji la Hongkhong huwa wanakutana mwezi wa juni na huku wakisema hakuna umuhimu wa kuoana.

Kwa mujibu wa tafiti ya mwaka 2013 iliyojikita zaidi katika masuala ya familia inayofanywa na baraza la familia la jiji la Hongkhong ni asilimia 60.3 ya watu wanaoishi katika jiji la Hongkhong wanaaamini kuwa suala la ndoa halina umuhimu katika maisha.

Tafiti hizo zinaendelea kujuza kuwa idadi ya wanaume na wanawake ambao hawajaowa na kuolewa imeongezeka katika miaka miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment