DEREVA mmoja wa
bodaboda aliyefahamika kwa jina la Ally Omary mwenye umri wa Miaka (29) amekufa
katika ajali iliyotokea barabara ya new Bagamoyo baada ya kugongana na gari la
kijeshi Lugalo.
Kamanda
wa polisi wa Wilaya ya Kinondoni Camilius Wambura amesema tukio hilo limetokea
hivi karibuni lango kuu la Lugalo jeshini barabara ya Bagamoyo Wilaya ya
Kinondoni .
Amesema
gari la kijeshi aina ya Iveco ambalo halikufahamika namba ya gari hilo na
dereva wake ilitokea upande wa barabara ya Lugalo jeshini hospitali na kwenda
upande wa pili kwa njia isiyoruhusiwa na kugongana na pikipiki hiyo. Pikipiki
yenye ya usajili T956 BAH ambapo kwa mujibu wa Wambura dereva wa gari hilo la
kijeshi ametoroka mara baada ya tukio hilo.

No comments:
Post a Comment