Tuesday, June 17, 2014

MKUU wa wilaya aagiza wenyeviti, wazazi na viongozi wa serikali kuchangia chakula shuleni


Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala 

MKUU wa wilaya ya Kilombero,mkoani Morogoro Hassan Masala amewaagiza wazazi,wenyeviti wa vijiji na viongozi wa serikali na sekta binafsi kuchangia chakula shuleni zoezi litakalo anza kuanzia Julai.


Katika hotuba ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyosomwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Iluminata Kapinga mjini Ifakara mkuu huyo alisema mpango huo unalengo la kuokoa zaidi ya watoto 47,423 katika shule za msingi 102.

Hata hivyo alikerwa na tabia ya walimu kutoripoti wakiwemo walimu 208 kati yao 119 wanawake na 89 wanaume kati ya walimu wa sekondari 233 wakiwemo wanawake138 na wanaume 98 waliotakiwa kuripoti mwaka huu wilayani humo.

Kuhusu umbali kutoka nyumbani hadi shuleni,mkuu huyo alisema mpango mkakati wa ujenzi hosteli umeanza ambapo hosteli nane zimejengwa na serikali na Mbili kujengwa na wazazi.

Akizungumzia hali ya vitabu alisema tayari serikali imefanikiwa kutoa hadi kufikia uwiano wa 1:1 nakuwa changamoto iliyobaki ni kwenye vitabu vya masomo ya sanaa ambayo itatatuliwa hivi punde.


No comments:

Post a Comment